TADIYE NI MRADI WA UWEZESHAJI WA VIJANA

KATIKA UJASIRIAMALI KWA KUTUMIA DIJITARI NA UBUNIFU TANZANIA

Pakua mfumo wa BESPAndiko Bora La Biashara

Andiko Bora la Wazo la Biashara - Sifa za Muombaji

  • Lazima awe mwanaume au mwanamke mwenye umri wa miaka 15-35
  • Lazima awe anatokea Tanzania Bara au Visiwani (Zanzibar)

  • Lazima awe anazungumza Kiingereza au Kiswahili

  • Lazima awe amejisajili na kupata mafunzo kupitia mfumo wa BESP na kukamilisha angalau masomo matano ikiwa ni pamoja na somo la Uandaaji wa Mpango wa Biashara
  • Wazo la biashara litakalowasilishwa lazima liwe na uwezo wa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kama chombo au kiwezeshi cha wazo hilo.
Omba Hapa
Andiko Bora  la Wazo  la   Biashara -  Sifa za Muombaji
MFUMO WA BESP

MFUMO WA BESP

BESP ni jukwaa la kujifunza mtandaoni ambalo linawawezesha wajasiriamali kupata ujuzi wa usimamizi wa biashara na kuwawezesha kuwa ubunifu katika kuboresha fursa zinazotolewa na uchumi wa digitali katika kuimarisha utajiri na uumbaji wa ajira.

PAKUA MFUMO

Kuhusu TADIYE

DTBI

DTBi: Ni atamizi iliyoanzishwa chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi (COSTECH) kama taasisi inayojitegemea kwa ajili ya kuwaendeleza vijana wenye ubunifu. Taasisi hii ilianzishwa ili kusaidia Tume katika kendeleza vijana wabunifu wenye mawazo endelevu ya kiubunifu na kiujasiriamali katika Tehama au kwa kutumia Tehama kama nyenzo katika kuendeleza vipaji vyao vya ubunifu.


TADIYE

Kuhusu TADIYE: Ni mradi wa kibunifu na kijasiriamali uliotengenezwa kwa ajili ya kutoa elimu ya ujasiriamali, kuhamasisha na kukuza biashara ndogo ndogo zinazotumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia simu kwa ajili ya vijana na kinamama waishio katika mazingira magumu. Mpango huu unatekelezwa na DTBi pamoja na wadau wengine wenye maono yanayofanana kwa ufadhili wa Ubalozi wa Denmark.

BESP

BESP: Ni mfumo uliopo ndani ya program ya TADIYE kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ujasirismali kwa vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-35. Mfumo huu pia utatumika katika kuendesha na kusimamia shindano la kutafuta mawazo bora ya biashara. Katika shindano hilo mawazo bora yasiopungua ishirini yatapatiwa ruzuku ya mtaji wa kati ya milioni 10-20 za kitanzania.