Andiko Bora la Wazo la Biashara – Sifa za Muombaji
- Lazima awe mwanaume au mwanamke mwenye umri wa miaka 15-35.
- Lazima awe anatokea Tanzania Bara au Visiwani (Zanzibar).
- Lazima awe anazungumza Kiingereza au Kiswahili.
- Lazima awe amejisajili na kupata mafunzo kupitia mfumo wa BESP na kukamilisha angalau masomo matano ikiwa ni pamoja na somo la Uandaaji wa Mpango wa Biashara.
- Wazo la biashara litakalowasilishwa lazima liwe na uwezo wa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kama chombo au kiwezeshi cha wazo hilo.
TADIYE NI MRADI WA UWEZESHAJI WA VIJANA
KATIKA UJASIRIAMALI KWA KUTUMIA DIJITARI NA UBUNIFU TANZANIA
MFUMO WA BESP
Ni mfumo uliopo ndani ya program ya TADIYE kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ujasirismali kwa vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-35.