WASHIRIKI WA SHINDANO LA ANDIKO LA BIASHARA WALIOCHAGULIWA KATIKA HATUA YA AWALI

Mradi wa uwezeshaji wa vijana (TADIYE) ni mradi wa kibunifu na kijasiriamali unaotekelezwa na Atamizi ya “DTBi” pamoja na washirika wengine wenye maono sawa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Denmark. Mradi huu umeanzishwa kwa lengo la kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili vijana hasahasa wanawake wadogo wanaoishi kwenge mazingira magumu kwa kuwapatia elimu na ujuzi wa kijasiriamali kupitia simu za mkononi. Kwa kupitia elimu hiyo ya ujasiriamali kwa njia ya simu vijana hao wanaweza kutumia fursa za uchumi wa kidigitali kutengeneza ajira, kujitengenezea kipato na kuongeza wingi wa biashara endelevu.
Tarehe 02/04/2019 Mradi wa TADIYE ulizindua Shindano la Andiko Bora la Biashara ambapo taarifa zilitolewa kupitia njia mbalimbali kama vile Tovuti ya mradi, magazeti, “App” ya BESP (Business Entrepreneurship Skills Platform) pamoja na mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter na Instagram). Shindano hilo lilikaa wazi kwa siku 21 (tarehe 02/04/2019 mpaka tarehe 23/04/2019) ili kutoa mda wa kutosha kwa walengwa Kushiriki.
Hadi kufikia tarehe ya mwisho ya watu kuwasilisha maombi yao (23/04/2019), Maombi 873 yalikuwa tayari yamekwishapokelewa kupitia mfumo maalum uliotengenezwa na mradi wa TADIYE kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Hata hivyo mfumo huo pia ulionyesha kuwa kuna watu wengine zaidi ya 1,800 ambao walijaribu kuwasilisha maombi yao bila mafanikio kutokana na kutokidhi vigezo vya awali kabisa vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo kupitia “APP” ya BESP na kufanikiwa kumaliza kusoma masomo yasiyopungua matano kati ya manane ikiwa ni pamoja na somo la Mpango wa Biashara.
Mradi wa TADIYE umekamilisha uchambuzi wa mawazo yote yaliyowasilishwa kikamilifu kutokana na vigezo zilivyokuwa vimewekwa ambapo tuumefanikiwa kupata washiriki 25 wa awali ambao watashiriki kwenye mafunzo ya siku tatu yatakayofanyika Dar-es-Salaam kuanzia siku ya Jumatano tarehe 13/6/2019 hadi tarehe15/6/2019. Tarehe 15/6/2019 kuanzia saa nane mchana washiriki watapata nafasi ya kuwasilisha mawazo yao kwenye jopo la majaji kwa ajili ya kuwapata washindi kamili.
Jedwali hapa chini linaonyesha majina ya vijana wenye Mawazo bora waliochaguliwa katika hatua ya awali kama ifuatavyo:
WALIOCHAGULIWA KATIKA HATUA YA AWALI: