UZINDUZI WA PROGRAMU YA KIATAMIZI
TANGAZO LA KUFUNGUA DIRISHA LA KUPOKEA MAOMBI
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Dar es salaam linapenda kuwatangazia umma wa watanzania ya kwamba imeanza kupokea maombi ya maeneo maalum ya kulea ubunifu (kiatamizi). Watakaochaguliwa watapata fursa ya kulea ubunifu wao kwa muda wa miaka mitatu (3) na baadaye kuhitimu. Kwa kipindi chote hicho watapewa mafunzo ya kuwajengea uwezo, watashiriki semina mbalimbali, wataunganishwa na taasisi za fedha na vilevile taasisi za elimu ya juu.Maelezo zaidi